Skip to main content Skip to footer

Kutowajibika Katika Uwekezaji: Agrica Ni Mfano Wa Mradi Wa Maendeleo Ulioharibika Tanzania

December 22, 2016

Mashamba ya kilombelo (KPL) yana ukubwa wa hekta 5,818 (ha) za mpunga zilizo katika kiini cha rutuba cha Bonde la Kilombero, Tanzania. Mbali na kuendeleza mashamba makubwa ya mpunga, KPL inafanya kazi na wakulima wadogo wadogo kupitia mashamba darasa yanayozingatia mfumo wa teknolojia ya ongezeko la mpunga (SRI) . Mradi wa uwekezaji unapata msaada mkubwa wa kifedha na kiufundi kutoka taasisi za maendeleo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Idara ya Kimataifa ya Maendeleo ya Uingereza (DfID) na USAID1. Ripoti hii inatoa matokeo ya uchunguzi uliofanywa Tanzania kati ya mwaka 2011 na 2015 ya mradi wa uwekezaji wa KPL, ukiangazia uzoefu unaopatikana katika jamii jirani.

Kutowajibika Katika Uwekezaji: Agrica Ni Mfano Wa Mradi Wa Maendeleo Ulioharibika Tanzania